• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 23, 2015

  HENRY AMKANDIA KINOMA CHICHARITO, ASEMA; "AMESHANGILIA KAMA AMESHINDA KOMBE LA DUNIA"

  GWIJI wa Ufaransa, Thierry Henry amekandia ushangiliaji wa Javier Hernandez 'Chicharito' baada ya kufunga bao la ushindi dakika za lala salama katika Robo Fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid akisema; "Kama ameshinda Kombe la Dunia'.
  Mshambuliaji huyo wa Real Madrid aliwanua mashabiki wa nyumbani kwa kufunga bao la ushindi baada ya kupokea pasi ya Cristiano Ronaldo zikiwa zimesalia dakika mbili baada ya kazi nzuri ya Mreno huyo.
  Nyota huyo wa Mexico, Hernandez akakikimbilia kwenye kona kushangilia peke yake baada ya kufunga, lakini Henry anafikiri mshambuliaji huyo wa mkopo kutoka Manchester United, 'amepora' sifa za mchezaji mwenzake.
  The on-loan Mexican striker wheels away in celebration as he fires Real Madrid in to the next round
  Javier Hernandez akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Real Madrid lililoipeleka Nusu Fainali

  Henry aliiambia Sky Sports: "Ili kutenda haki kwake, hakucheza haswa. Alipewa nafasi usiku huu, lakini bado hatujui kama atacheza tena.
  "Alipata nafasi kadhaa katika mchezo. Moja katika mguu wake wa kushoto na kisha nyingine katika mguu wake wa kulia. Lakini naweza kukuambia, anahitaji kumshukuru (Cristiano) Ronaldo usiku huu.
  "Nafahamu alikwenda kushangilia peke yake na kila kitu, lakini anahitaji kumshukuru Ronaldo, kwa sababu kwangu alichangia pia. Ni Ronaldo ambaye alichagua kubadilisha mwelekeo wa mchezo.
  Hernandez falls backwards in celebration after his late goal earned Real Madrid a Champions League victory
  Hernandez akiteleza kwenye nyasi kushangilia bao lake lililoipeleka Real Madrid Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa

  "Alimuona jamaa katika nafasi nzuri, ambaye alikuwa ni Hernandez, na akampa mpira, hivyo hilo ni bao la Ronaldo. Ambacho sijapenda ni ushangiliaji wake kama ameshinda Kombe la Dunia. Alitakiwa kufunga na kugeuka kushangilia na Ronaldo.
  Thierry Henry was quick to criticise the Mexican striker for the way in which he celebrated his winner
  Thierry Henry haraka alimshambulia mshambuliaji huyo wa Mexico kwa namna alivyoshangilia bao lake jana

  Kwa upande wake, beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher na mchambuzi mwenzake Henry, pamoja na kusema Ronaldo ni mbinafsi, lakini akamsifu kwa alichokifanya kwani ndicho alipaswa kufanya kwa manufaa ya timu.
  "Lilikuwa bao la Ronaldo kwa maana ya jitihada alizofanya kupatikana kwa bao lile, lakini Ronaldo ni wa ovyo zaidi duniani katika mambo kama yale. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HENRY AMKANDIA KINOMA CHICHARITO, ASEMA; "AMESHANGILIA KAMA AMESHINDA KOMBE LA DUNIA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top