• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 28, 2015

  MALINZI AWAVISHA RASMI YANGA SC UBINGWA NA PONGEZI JUU, WAPINZANI WALIE TU

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji kufuatia timu yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2014/2015.
  Katika salamu zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani.
  Klabu ya Yanga SC imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu nchini kwa mara ya 24 (ishirini na tano) jana, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Polisi Morogoro katika uwanja wa Taifa huku ikiwa na michezo miwili mikononi kabla ya ligi kumalizika.

  Waziri wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo, Dr. Fennela Mkangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Mei 6, 2015 katika mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINZI AWAVISHA RASMI YANGA SC UBINGWA NA PONGEZI JUU, WAPINZANI WALIE TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top