• HABARI MPYA

  Sunday, April 26, 2015

  CHELSEA YATOKA SALAMA EMIRATES, UBINGWA WIKI IJAYO

  Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas kulia akimdhibiti mshambuliaji wa timu yake ya zamani, Arsenal, Olivier Giroud katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Emirates, London. Timu hizo zimetoka 0-0. Chelsea inafikisha pointi 77 baada ya kucheza medhi 23 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 67 za mechi 34. Hii maana yake, Chelsea inaweza kutangaza ubingwa wiki ijayo ikishinda dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Stamford Bridge Mei 3, kwani itafikisha pointi 80 ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani kwa mujibu wa mechi zilizobaki.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YATOKA SALAMA EMIRATES, UBINGWA WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top