• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 25, 2015

  AZAM FC ‘WABOMOA BENKI’ KULETA STRAIKA LA KUSHIKISHA ADABU BARA

  Mohamed Traore anakuja Azam FC
  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BODI ya Azam FC imekubali kwa moyo mkunjufu kubomoa benki kumleta mshambuliaji wa kushikisha adabu wapinzani.
  Huyo si mwingine zaidi ya mshambulaji wa kimataifa wa Mali, Mohamed Traore ambaye kwa sasa anachezea El Merreikh ya Sudan.
  BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba Traore ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Mali kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka huu Equatorial Guinea, amekubali kuhamishia cheche zake Azam FC. 
  Azam FC ilijaribu bila mafanikio katika dirisha dogo Desemba mwaka jana kumsajili Traore, lakini ikashindwa dau la El Merreikh, licha ya kuwa imekwishakubaliana na mchezaji mwenyewe.
  Ila kwa sasa Azam FC ikiwa inaelekea kabisa kupoteza ubingwa wa Ligi Kuu, bodi imeamua kuboresha kikosi kujiimarisha kwa mapambano ya msimu ujao.
  Wakurugenzi wa Azam FC, Abubakar Bakhresa na Yussuf Bakhresa, wote ni mashabiki wa Traore 

  Mkurugenzi Mkuu wa Azam FC, Abubakar Bakhresa na mdogo wake, Yussuf Bakhresa wote ni mashabiki wakubwa wa Traore na hiyo pekee inaashiria wakati wa mshambuliaji huyo kujiunga na timu ya Chamazi umewadia.
  Na beki Serge Wawa raia wa Ivory Coast aliyekuwa naye Traore El Merreikh kabla ya kutua Azam FC Desemba, amekuwa kishawishi kikuu cha klabu hiyo kuifukuzia saini ya Mmali huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC ‘WABOMOA BENKI’ KULETA STRAIKA LA KUSHIKISHA ADABU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top