• HABARI MPYA

  Monday, April 27, 2015

  SC VILLA, KCC ZANUKIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  Na Musa Mugabi, KAMPALA
  VIGOGO wa soka Uganda, SC Villa na KCC FC wote wameanza na ushindi katika mechi zao za kwanza za Nusu Fainali ya Kombe la Uganda jana.
  Timu zote zimepata ushindi sawa, wa 1-0, SC Villa wakiwafunga BUL FC Uwanja wa Kakindu katika mji mdogo wa Jinja wakati KCC imeifunga Lweza FC katika Uwanja wa kumbukumbu wa Philip Omondi.
  Bao la SC Villa lilifungwa na Denis Kamanzi wakati la KCC lilifungwa na Herman Wasswa. Mechi za marudiano zitachezwa Mei 3, 2015 na washindi watakutana katika fainali. 
  Lweza watakuwa wenyeji wa KCC FC Uwanja wa Mutessa II, huko Wankulukuku wakari SC Villa na BUL zitapepetana Uwanja mkongwe wa Nakivubo katikati ya Jiji la Kampala.
  Bingwa wa Kombe la Uganda huiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SC VILLA, KCC ZANUKIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top