• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 25, 2015

  NUSU FAINALI KOMBE LA UGANDA; SC VILLA NA BUL, KCC NA LWEZA

  KCC ya Uganda itamenyana na Lweza Jumapili katika Nusu Fainali ya Kombe Uganda, wakati SC Villa itamenyana na BUL.
  Hiyo inafuatia droo ya Nusu Fainali iliyofanyika juzi katika ofisi Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Mengo mjini Kampala.  Mechi za marudiano zinatarajiwa kufanyika Jumapili ya Mei 3, mwaka huu.
  URA ndiyo wafalme wa michuano hiyo, baada ya kushinda taji hilo kwa msimu wa 2013/2014 mjini Mbale kufuatia kuifunga KCC katika fainali.
  Mshindi wa taji la Uganda Cup huiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NUSU FAINALI KOMBE LA UGANDA; SC VILLA NA BUL, KCC NA LWEZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top