• HABARI MPYA

    Sunday, April 12, 2015

    STAND UNITED YAIPIGA 1-0 POLISI NA KUTUA ANGA SALAMA

    Na Philip Chimi, SHINYANGA
    STAND United imezidi kujiwekea mazingira ya kubaki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro jioni ya leo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
    Shukrani kwake Mnigeria, Abasalim Chidiebele aliyefunga bao hilo pekee kwa penalti dakika ya 56 baada ya beki wa Polisi kumchezea rafu mshambuliaji wa Stand, Pastory Athanas.

    Stand sasa inatimiza pointi 27 baada ya kucheza mechi 21 na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya 11.
    Kikosi cha Stand United kilikuwa; John Mwenda, Revocutus Richard, Abuu Ubwa, Jisend Maganga, Peter Mutabuzi, Reyna Mgungila, Pastory Athanas/Thola Anthony, Hamisi Shengo, Heri Mohamed/John Ngaga, Abasalim Chidiebele na Haroun Chanongo.
    Polisi Moro; Elias Sospeter, Ally Teru, Simon Fanuel, Meshack Abel, Laban Kambole, Said Mkangu, Bantu Admin, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Imani Mapunda/Edward Christopher, Mussa Mohammed/Nahoda Haji na Salum Kihimbwa/Edger Charles.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED YAIPIGA 1-0 POLISI NA KUTUA ANGA SALAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top