• HABARI MPYA

    Sunday, April 12, 2015

    SHETANI HILI SASA BALAA, MAN UNITED YAIKUNG’UTA CITY 4-2

    UBISHI umeisha. Manchester United ndiyo wakali wa Manchester, baada ya jioni ya leo kuwafunga mahasimu wao wa Jiji, Manchester City mabao 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafrord. 
    Ushindi huo, unaifanya sasa City izike matumaini ya kutetea ubingwa- lakini pia kujiweka katika mazingira magumu hata kupata nafasi ya pili.
    United ya Louis Van Gaal, sasa inafikisha pointi 65 baada ya kucheza mechi 32, sawa na City yenye pointi 61. Arsenal ni ya pili kwa pointi zake 66 za mechi 32 pia, wakati Chelsea ipo kileleni kwa pointi zake 73 za mechi 31.
    All of United's outfield players congratulate Chris Smalling after his close-range header sealed the rout
    Wachezaji wote wa Manchester United, wakimpongeza Chris Smalling baada ya kufunga bao la nne

    City walikuwa wa kwanza kupata bao leo, lililofungwa na Sergio Aguero dakika ya nane, akimalizia krosi ya David Silva, kabla ya Ashley Young kuisawazishia United dakika sita baadaye baada ya kukutana na mpira uliokuwa unaelea kwenye boksi. 
    Marouane Fellaini akaunganisha krosi ya Young kuifungia United bao la pili dakika ya 28 na la sita kwake msimu huu, kabla ya Juan Mata kutumia ubutu wa safu ya ulinzi ya City kuifungia United bao la tatu dakika ya 66.
    Chris Smalling aliyekuwa amesahaulika, akamalizia mpira wa adhabu wa Young kuipatia United bao la nne dakika ya 73 kabla ya Aguero kumalizia krosi ya Pablo Zabaleta kuifungia bao la pili Man City dakika ya 89.
    Vincent Kompany alimchezea rafu Daley Blind na kusababisha mzozo hadi akapewa kadi ya njano, kabla ya kutolewa mapumziko.  
    Huo unakuwa ushindi wa sita mfululizo kwa Mashetani Wekundu katika Ligi Kuu, ambayo ni rekodi ya kuvutia baada ya muda mrefu.
    Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia, Smalling, Jones/Rojo dk75, Blind, Carrick, Mata/Di Maria dk81, Ander Herrera, Fellaini/Falcao dk83, Young na Rooney.
    Manchester City; Hart, Zabaleta, Kompany/Mangala dk46, Demichelis, Clichy, Jesus Navas/Lampard dk73, Toure, Fernandinho, Milner/Nasri dk63, Silva na Aguero.
    Ashley Young latches on to a loose ball and fires past the despairing dive of Hart to level matters
    Ashley Young akiifungia bao la kwanza United ambalo lilikuwa la kusawazisha kabla ya kuibuka na ushindi wa 4-2

    PICHA ZAIDI NENDA: 

    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3035938/Manchester-United-4-2-Manchester-City-Ashley-Young-Marouane-Fellaini-Juan-Mata-Chris-Smalling-target-Red-Devils-run-riot.html#ixzz3X7DizrHh
    Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHETANI HILI SASA BALAA, MAN UNITED YAIKUNG’UTA CITY 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top