TIMU ya Real Madrid imeshinda mabao 3-0 katika La Liga leo dhidi ya Eibar na kupunguza pengo la pointi inazozidiwa na vinara, Barcelona hadi kubaki moja, japo kwa muda.
Real sasa inafikisha pointi 73 baada ya kucheza mechi 31, wakati Barca inacheza mechi yake ya 31 dhidi ya Sevilla hivi, mchezo ukiwa unaelekea mwishoni, inaongoza 2-1- ikishinda itaendelea kuongoza kwa pointi nne zaidi.
Cristiano Ronaldo alianza kuifungia Madrid kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 21 Uwanja wa Bernabeu, kabla ya Javier Hernandez kufunga la pili dakika ya 31 na Jese la tatu dakika ya 83.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Navas, Arbeloa, Varane, Ramos/Pepe dk64, Marcelo/Nacho dk65, Modric/Borges dk61, Illarramendi, Isco, Jese, Hernandez na Ronaldo.
Eibar: Xabier Irureta, Castellano Castro, Anibarro, Rodriguez Navas, Vila Rosello Booked, Fernandez, Garcia, Carrillo/Boateng dk77, Capa, Berjon Perez/Arruabarrena dk45, Lara Grande na Del Moral Fernandez/Piovaccari dk66.
Cristiano Ronaldo akiwatupia busu mashabiki Uwanja wa Santiago Bernabeu baada ya kuifungia Real Madrid bao la kwanza
PICHA ZAIDI NENDA:
http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3034934/Real-Madrid-3-0-Eibar-Cristiano-Ronaldo-ends-free-kick-goal-drought.html#ixzz3X1ud18ty


.png)
0 comments:
Post a Comment