• HABARI MPYA

    Saturday, April 11, 2015

    ARSENAL ‘WAITIA PRESHA’ CHELSEA KILELENI, WAICHAPA BURNLEY 1-0 NA KUJIVUTA TENA

    TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Burnley Uwanja wa Turf Moor katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
    Shukrani kwake kiungo Aaron Ramsey, aliyeifungia bao hilo pekee The Gunners mapema dakika ya 12 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua. 
    Ushindi huo wa nane mfululizo katika Ligi Kuu, unaifanya Gunners ipunguze idadi ya pointi inazozidiwa na vinara Chelsea hadi kubaki nne. Chelsea ina pointi 70, baada ya kucheza mechi 30, wakati Arsenal ina pointi 66 za mechi 32, ikifuatiwa na Manchester United pointi 62 mechi 31, ambayo kesho itamenyana na mahasimu Manchester City wenye pointi 61 mechi 31 pia.  
    Burnley inazidi kutitia mkiani, sasa ikishika nafasi ya pili kutoka mkiani, kwa pointi zake 26 za mechi 32, mbele ya Leicester City pointi 25 mechi 31.  Kikosi cha Burnley kilikuwa; Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Arfield, Jones/Taylor dk90, Boyd, Barnes, Ings na Vokes.
    Arsenal; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Carzola, Ramsey, Ozil, Sanchez/Chambers dk90 na Giroud/Welbeck dk82.
    Ramsey is congratulated by Arsenal team-mates Olivier Giroud (left) and Hector Bellerin after his early goal
    Aaron Ramsey akipongezwa na wachezaji wenzake wa Arsenal, Olivier Giroud (kushoto) na Hector Bellerin baada ya kufunga bao pekee leo la ushindi

    PICHA ZAIDI NENDA: 

    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3035022/Burnley-0-1-Arsenal-Aaron-Ramsey-s-12th-minute-strike-Arsene-Wenger-s-close-gap-leaders-Chelsea.html#ixzz3X1qvws5n 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL ‘WAITIA PRESHA’ CHELSEA KILELENI, WAICHAPA BURNLEY 1-0 NA KUJIVUTA TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top