• HABARI MPYA

    Sunday, April 12, 2015

    RAHEEM STERLING KWISHA HABARI YAKE, AMEANZA KUVUTA SHISHA!

    WINGA wa Liverpool, Raheem Sterling hana uzito wa kupamba sana kurasa za mwisho za magazeti, lakini kwa mara nyingine leo ameteka kurasa hizo kufuatia kupigwa picha akiwa anavuta bomba la shisha.
    Katika picha iliyitolewa na gazeti la Sunday Mirror, kinda huyo wa miaka 20 anaonekana akivuta shish yenye dawa za kulevya katika bomba la rangi ya chungwa, ambalo ndani yake lina matunda na tumbaku na anavuta kwa ufahari.
    Sterling hivi karibuni alikataa mshahara Pauni 100,000 kwa wiki kusaini Mkataba mpya Anfield akisema ana njaa ya mataji kuliko fedha, jambo ambalo limezua wasiwasi anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu. 
    Liverpool midfielder Raheem Sterling can be seen pictured on social media whilst smoking a shisha pipe
    Kiungo wa Liverpool, Raheem Sterling akivuta bomba la shisha
    The England international (right) played in the Red's FA Cup quarter final win over Blackburn on Wednesday
    Kinda huyo wa kimataifa wa England (kulia) aliiongoza Liverpool kuitoa Blackburn katika Robo Fainali ya Kombe la FA Jumatano

    Sterling, ambaye ameichezea mechi 14 tu England, alipi9gwa picha akivuta shisha na kupostiwa kwenye mitandao ya kijamii ikiambatana na maelezo; ‘1 down 3 to go’, maana yake alikuwa akimaliza hiyo anapiga nyingine tatu.
    Inasemekana shisha moja ni sawa na kuvuta sigara 200, maana yake kinda huyo hatakuwa na maisha marefu ya kucheza soka ya kiwango cha juu iwapo hataacha 'ushamba huo'.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAHEEM STERLING KWISHA HABARI YAKE, AMEANZA KUVUTA SHISHA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top