• HABARI MPYA

    Sunday, April 12, 2015

    NDUMBARO AILAMBA CHENGA TFF, LAKINI KUULI BADO ANAYE TU, AMPA WITO WA MWISHO, ASIPOTOKEA IMEKULA KWAKE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeshindwa kujadili rufaa ya Dk Damas Numbaro, kwa sababu hakutokea katika kikao kilichofanyika leo.
    Mwenyekiti, Revocatus Kuuli amesema kwamba leo walitaraji kujadili rufaa namba 1/2014 ya Dk. Ndumbaro dhidi ya TFF, lakini kwa bahati mbaya mlalamikaji hakufika.
    Kuuli amesema upande wa TFF, mwakilishi wake Wakili Msomi Emmanuel Muga alifika na kufuatia kutofika kwa Dk. Ndumbaro, Kamati yake, imeagiza TFF itoe wito mpya hadi Aprili 14, mwaka 2015 uwe umemfikia mlalamikaji huyo na afike katika kikao kijacho cha kusikiliza rufaa yake.
    Ndumbaro amekata rufaa kupinga kufungiwa na TFF miaka saba kutojihusisha na mambo ya soka, baada ya kukutwa hatia za kimaadili.
    Dk Damas Ndumbaro hakutokea kikao cha Kamati ya Rufaa leo, lakini ataitwa tena

    Ndumbaro aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Jamal Malinzi baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
    Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDUMBARO AILAMBA CHENGA TFF, LAKINI KUULI BADO ANAYE TU, AMPA WITO WA MWISHO, ASIPOTOKEA IMEKULA KWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top