KLABU ya Manchester United itampa Robin van Persie ofa ya Pauni Milioni 5 ili aondoke katika klaabu hiyo mwishoni mwa msimu.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 31, amebakiza miezi 14 katika mkataba wa mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki Old Trafford, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu uongozi wa United uko tayari kumlipa nusu ya Pauni Milioni 10 za mafao yake— awaliyokubaliana wakati anasaini kutoka Arsenal mwaka 2012 — ili aondoke.
Vigogo wa Italia, Juventus na Inter Milan zote zimekuwa zikihusishwa na kumtaka Mholanzi huyo na United iko tayari kuendelea kumlipa nusu ya mshahara Van Persie, ili nyingine alipwe na klabu iyakayomchukua kati ya vigogo hao wa Serie A.
Mshambuliaji huyo wa Uholanzi amekuwa katika wakati mgumu Man United, kutokana na kuandamwa na majeruhi- lakini amemudu kufunga mabao 10 katika Ligi Kuu
Mchezaji anayetakiwa Manchester United, Memphis Depay anatazamiwa kuondoka PSV mwishoni mwa msimu
Lazio pia inamtaka. Radamel Falcao na Javier Hernandez pia wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu, wakati United imekuwa ikihusishwa na mpango wa kutaka kuwachukua washambuliaji wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani na Memphis Depay wa PSV ya Uholanzi.
Timu ya Louis van Gaal inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Lig Kuu ya England na leo inamenyana na mahasimu, Manchester City Uwanja wa Old Trafford, mchezo ambao wakishinda watakuwa kwanawazidi wapinzani hao kwa pointi nne.


.png)
0 comments:
Post a Comment