Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MAREFA kutoka Msumbiji ndiyo watachezesha mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga SC na Etoile du Sahel Jumamosi wiki hii.
Yanga SC wanaanzia nyumbani kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano hiyo, na baada ya kuzitoa BDF XI ya Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe, Jumamosi watavaana na Etoile ya Tunisia.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua marefa wa Msumbiji kuchezesha mechi hiyo Dar es Salaam.
Marefa hao ni Samuel Chirindza atakayepuliza filimbia akisaidiwa na wapeperusha vibendera, Arsenio Chadreque Marengula na Celio de Jesus Mugabe.
Yanga SC inatarajiwa kuingia kambini leo kuanza rasmi maandalizi ya mchezo huo, baada ya jana kundeleza wimbi la ushindi katika mechi ya sita mfululizo ya Ligi Kuu.
Yanga SC jana iliifunga Mbeya City mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Kpah Sherman, Salum Telela na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

![]() |
| Marefa wa Msumbiji wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kuanzia Jumatano kuja kuchezesha mechi ya Yanga na Etoile |
Marefa hao ni Samuel Chirindza atakayepuliza filimbia akisaidiwa na wapeperusha vibendera, Arsenio Chadreque Marengula na Celio de Jesus Mugabe.
Yanga SC inatarajiwa kuingia kambini leo kuanza rasmi maandalizi ya mchezo huo, baada ya jana kundeleza wimbi la ushindi katika mechi ya sita mfululizo ya Ligi Kuu.
Yanga SC jana iliifunga Mbeya City mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Kpah Sherman, Salum Telela na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
%2B%2BMauritius%2B%2B%2Bvs.%2B%2BMauritania%2B%2B%2B-%2BChirindza%2B(Mozambique).jpg)

.png)
0 comments:
Post a Comment