Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI Mliberia wa Yanga SC, Kpah Sean Sherman jana amefunga katika mechi ya pili mfululizo, baada ya ukame wa mabao tangu Januari, hata hivyo aliumia kipindi cha pili na kutolewa nje.
Sherman alifunga bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar s Salaam.
Hata hivyo, kipindi cha pili Mliberia huyo aliomba mwenyewe kutoka wakati Mrisho Ngassa ameitwa kwenda kumbadili Simon Msuva. Ilibidi badala ya kutolewa Msuva, atolewe Sherman kumpisha Ngassa.
Mliberia huyo alitoka uwanjani akiwa anachechemea wakati anampisha Ngassa na baada ya mechi akaiambia BIN ZUBEIRY nyonga bado inamsumbua.
Maumivu ya nyonga yamemfanya Sherman awe adimu katika kikosi cha Yanga SC siku za karibuni na haijulikani baada ya kuumia tena jana itamchukuaa muda gani kuejea uwanjani.
Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm atahitaji wachezaji wake wote wawe fiti kuelekea mechi na Etoile du Sahel mwishoni mwa wiki.
Yanga SC watakuwa wenyeji wa Etoile Aprili 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Sherman amesema; “Nyonga bado inanisumbua. Sikutaka kuendelea kuwa uwanjani ili nisiiumize zaidi, ngoja nione nitaamkaje kesho,”alisema jana Sherman.

![]() |
| Mshambuliaji Mliberia wa Yanga SC, Kpah Sherman jana alifunga bao, lakini akatoka anachechemea kipindi cha pili kwa maumivu ya nyonga |
![]() |
| Sherman alicheza vizuri jana, kama ambavyo inaonekana hapa akimuacha Juma Nyosso |
Mliberia huyo alitoka uwanjani akiwa anachechemea wakati anampisha Ngassa na baada ya mechi akaiambia BIN ZUBEIRY nyonga bado inamsumbua.
Maumivu ya nyonga yamemfanya Sherman awe adimu katika kikosi cha Yanga SC siku za karibuni na haijulikani baada ya kuumia tena jana itamchukuaa muda gani kuejea uwanjani.
Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm atahitaji wachezaji wake wote wawe fiti kuelekea mechi na Etoile du Sahel mwishoni mwa wiki.
Yanga SC watakuwa wenyeji wa Etoile Aprili 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Sherman amesema; “Nyonga bado inanisumbua. Sikutaka kuendelea kuwa uwanjani ili nisiiumize zaidi, ngoja nione nitaamkaje kesho,”alisema jana Sherman.

.png)
0 comments:
Post a Comment