Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba mikataba yao ya sasa waliyoingia na wachezaji wao, inawapa fursa ya kuwatema bila malipo, iwapo watashuka viwango.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY katika mahojiano maalum jana Dar es Salaam, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba baada ya kuona wanapata hasara kutokana na wachezaji wazembe, wakalazimika kutengeneza mikataba salama zaidi kwao.
“Sisi kama klabu tunasajili mchezaji ili atusaidie na ndiyo maana tunatumia fedha nyingi, haswa kwa hawa wachezaji wa kigeni. Lakini unamleta mtu katika timu anashindwa kufanya juhudi za kuisaidia timu,”.
“Ukisema umuache ili usajili mwingine, tena bila kujali kama ulimlipa fedha nyingi kiasi gani, anataka alipwe na fidia ya mishahara ya kipindi chote kilichobaki cha Mkataba aliosaini.
Na tumeingia hasara za namna hiyo nyingi tu. Kwanza ile tu kumsajili mchezaji kwa Mkataba wa miaka miwili kwa mfano, halafu baada ya miezi sita unaamua kumuacha, pekee ni hasara kubwa. Lakini unapomuacha anakushitaki hadi FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) umlipe fedha zaidi,”amesema Poppe.
Kutokana na hali hiyo, Poppe amesema kwamba walichimba zaidi FIFA kuhusu namna ya kuepukana na matatizo ya aina hiyo, wakagundua dawa ni kuboresha mikataba,”.
“Iko wazi hata FIFA, unapomsajili mchezaji katika Mkataba mnaandikiana kabisa, kama akishindwa kuonyesha uwezo na kocha akathibitisha, basi Mkataba utavunjwa bila malipo ya ziada,”amesema.
Poppe amewataka wachezaji wote wa Simba SC kuzingatia hilo na kuhakikisha wanakuwa katika viwango vizuri wakati wote ili waisaidie timu, vinginevyo ripoti ya kocha ikidhihirisha mchezaji ameshuka kiwango, ataachwa bila fidia.
“Na wao wanalijua hilo, kwa sababu katika Mikataba yao hiyo ipo. Sasa sisi tutasubiri ripoti ya mwalimu tu, akituambia mchezaji huyo ameshuka kiwango kuanzia asilimia 30 tutamuacha na ataondoka bila malipo ya ziada,”amesema.
Poppe amesema waliingia katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu kwa ajili ya kushiriki kuipa uzoefu timu, ili msimu ujao ndiyo wawanie ubingwa.
Hata hivyo, amesema kulingana na mwenendo wa ligi hiyo hadi sasa, wanaona iwapo watafanya vizuri katika michezo yao iliyobaki wanaweza japo kupata nafasi ya pili.
“Azam FC wamelegalega, tunaona kabisa hata nafasi ya pili tukiongeza bidii tutaichukua. Tayari tumeweka dhamira ya kupambana tupate hiyo nafasi,”amesema.
Poppe amesema walijipanga kurudi kwenye michuano ya Afrika mwaka 2017, lakini sasa wanatamani kurejea kwenye anga hizo mwakani, baada ya Azam FC kupoteza mwelekeo.
Mabingwa hao watetezi, Azam FC wana pointi 38 katika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 20, wakati Simba SC ni ya tatu kwa pointi zake 35 za mechi 21. Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21, wapo kileleni.

![]() |
| Hans Poppe amesema kwamba mchezaji mzembe watamuacha bila fidia |

| Simon Sserunkuma bado hajaonyesha umuhimu wake Simba SC |
![]() |
| Dan Sserunkuma alisajiliwa kwa kishindo Simba SC, lakini mwendo wake ni wa kusuasua, ingawa wengi wanashauri apewe muda |
Hata hivyo, amesema kulingana na mwenendo wa ligi hiyo hadi sasa, wanaona iwapo watafanya vizuri katika michezo yao iliyobaki wanaweza japo kupata nafasi ya pili.
“Azam FC wamelegalega, tunaona kabisa hata nafasi ya pili tukiongeza bidii tutaichukua. Tayari tumeweka dhamira ya kupambana tupate hiyo nafasi,”amesema.
Poppe amesema walijipanga kurudi kwenye michuano ya Afrika mwaka 2017, lakini sasa wanatamani kurejea kwenye anga hizo mwakani, baada ya Azam FC kupoteza mwelekeo.
Mabingwa hao watetezi, Azam FC wana pointi 38 katika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 20, wakati Simba SC ni ya tatu kwa pointi zake 35 za mechi 21. Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21, wapo kileleni.

.png)
0 comments:
Post a Comment