• HABARI MPYA

    Sunday, April 12, 2015

    KIKAPU MWANZA CHAHITAJI KUPIGWA JEKI ILI KUINUKA

    Na Alex Sanga, MWANZA
    MKOA wa Mwanza una timu 11 za wanaume Mpira wa kikapu Timu hizo ni Bugando Planet, Bugando Warriors na Bugando Heats zote zipo kata ya Bugando, Nyakato Blandons ya Nyakato, Pasians Dolphin, Mwanza Eagles.
    Timu za wanawake zipo 2 tu Polisi queens ya Mabatini na shule ya Waschana Loreto. Timu ya chuo ya Saut,The Punisher kutoka wilaya ya Magu, Butimba Spiders ya kata ya Butimba,Bablon Force kutoka Ngudu na St Francis ya
    Nyakahoja Chama cha Mpira wa kikapu Mkoani Mwanza (MRBA) kipo Bado katika hali tata sana ya kuweza kujiendesha ili kiweze kuokoa Mchezo huu wa Mpira
    wa kikapu ambao Unapoteza thamani yake.
    MRBA inachangamoto kubwa zifuatazo chama cha Mpira wa kikapu hakina Uwanja wake binafsi imekuwa ikitegemea viwanja vya Tasisi kama chuo cha Mtakatifu Agustino na chuo cha Uwalimu Butimba.
    Viwanja hivi ndio vyenye ahueni kidogo na kila ligi ya Mpira wa kikapu inapoanza huchezwa hapo na Uwanja wa BOT uliopo maeneo ya pasiansi.
    Ukosefu wa wakufunzi wa kutosha Mfano Walimu waliosomea Mchezo huo. MRBA ina walimu wanne tu wenye utaalamu na huu Mchezo ambao ni Benson Nyasebo, Juvenile Kaiza, Aidan Abdul na Shomari Almasi.
    Timu za Mpira wa kikapu Hazina vifaa vya kutosha kama
    jezi,Viatu,Mpira.Timu nyingi Hazina fedha za kutosha ili Kuweza Kulipa viingilio katika ligi ya Mkoa ambacho ni shilingi Elfu 50,000/=.
    Timu pia hazina nidhamu katika Mech unakuta baadhi ya timu zinagomea kufika Uwanjan zikisingizia Hazina Nauli timu Kama ya Mwanza Eagles iliweza kugomea kufika uwanjan katika Mechi ya ligi ya Mkoa kati ya Mwanza Eagles na Butimba spiders desemba Mwaka jana katika uwanja wa
    chuo cha saut ambapo ligi ya Mkoa bado inachezwa.
    Viwanja Bado changamoto pia timu zenye viwanja vyao ni Mwanza Eagles ambayo ina kiwanja Kilmahewa,Pasians Dolphins ina kiwanja chake.
    Wachezaji wa Planet wakifurahia taji lao


    MRBA haina Mashindano ya kuinua vipaji tena kama ilvyokuwa Mwaka 2011 kulikuwa na mashindano ya kuinua vipaji Mashuleni haswa shule za sekondari ambapo shule za sekondari za Pamba, Mwanza Sekondari, Lake, Taqwa na Thaqafa zilikuwa zikifanya vyema katika mashindano hayo.
    Licha ya hivyo, pia mashindano ya Inter College hayaendelei tena tokea Mwaka 2007. Mashindano haya yalihusisha vyuo vya Mtakatifu Agustino, Chuo cha Uvuvi (Fisheries), CBE na Chuo cha Uwalimu Butimba.
    Mashindano yote ya Intercollege na sekondari Yalifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba chini ya udhamini wa kinywaji cha Sprite. Ukosefu wa wadhamini bado changamoto Wadhamini wengi hawa udhamini huu
    Mchezo Mpaka sasa kuna Mdhamini Mmoja tu ambae ni Al hitafi Hirani Mwenye sheli za Moil.
    Licha ya changamoto hizo pia chama cha Mpira wa Kikapu kimefanikiwa katika Kushiriki Mashindano ya Taifa Cup ambayo yapo Katika usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa kikapu taifa (TBF) Kupitia Mchezo wa Mpira wa kikapu watu wameweza kupata ajira mfano Ashirafu Haruna alipata kazi JKT Kigoma, Frank Maengela naye alienda jeshini pia.
    Pengine shirikisho la Mpira wa kikapu Taifa (TBF) lingerudisha Taifa Cup, ambayo ingekuwa na uwezo wa kushirikisha Mikoa yote ya Tanzania na kuweka Msisitizo Katika Ligi ya Mkoa na Kujenga Viwanja vya Mchezo
    Huu.
    Serikali ijenge academi zitakazo wafunza vijana Mchezo huu na pia kutoka Mafunzo Malumu kwa Makocha na Refree.
    Miaka ya Nyuma timu ya Wanaume ya Mpira wa kikapu ya Bugando Planet ilikuwa na Wachezaji wa mpira wa kikapu ambayo ilishiriki katika Mashindano ya Klabu bingwa Zanzibar 2004.
    Bugando Planet iliundwa na Vicent Shinda,Francis Shilindi, Amri Mohamed, Wilson Masanja, Prosper Mazigo, Apolo Katole, Bavon Mazigo, Mdace Makula, Micheal Mwita, Abdul Juma.
    Timu ya wanaume ya mpira wa kikapu ya Mwanza pia ilishiriki Michuano ya Afrika Mashariki yaliofanyika Mombasa (2007) na Uganda (2005).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIKAPU MWANZA CHAHITAJI KUPIGWA JEKI ILI KUINUKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top