• HABARI MPYA

    Monday, April 13, 2015

    'DEBI' LA MASHEMEJI KENYA LAISHIA SARE

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    BINGWA mtetezi wa ligi kuu Kenya, KPL, Gor Mahia imekamatwa na hasimu wake wa jadi AFC Leopards 1 – 1 kwenye mechi kali iliyopigwa alasiri ya Jumapili katika uwanja wa taifa wa Nyayo.
    Victor Ali Abondo aliipa Gor uongozi dakika ya 35 akimalizia krosi ya Mganda Khalid Aucho huku Mrwanda Meddie Kagere akikosa nafasi za kuhesabika kuongeza idadi ya mabao kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika.
    Kipindi cha pili, kocha wa Leopards Zdravko Logarusic alikipiga jeki kikosi chake katika safu ya kati kwa kumleta mchezoni Bernard Mang’oli na kumtoa Mganda Musa Mudde ndiposa Chui wakazawazisha dakika tano baadaye kupitia Jacob Keli aliyesukumiza mpira nyavuni baada ya mlindamlango wa Gor Boniface Oluoch kushindwa kunyaka shuti la Mrundi Emmanuel Ngama kufuatia pasi ya raia wa Nigeria Austine Ikkena upande wa kulia.

    Timu zote zikipoteza nafasi za kuongeza bao hadi dakika ya mwisho mwamuzi Nassur Doka alipopuliza kipienga kuashiria sare ambayo inawasalisha K’Ogalo kileleni mwa jedwali kwa alama 13, nne zaidi ya nambari saba AFC Leopards ambao wamecheza mechi sita, moja kumliko Gor.
    Vijana wa Frank Nuttal wameshinda taji la ligi kuu mara 14 hivi karibuni mwaka 2013 na 2014 huku Leopards wakiliwai mara 1, mwisho mwaka 1998 na ni timu mbili kuu katika historia ya soka nchini Kenya. Tusker ameliwai mara kumi huku Ulinzi Stars akishinda mara nne tu.
    Uwanjani Afraha, bingwa mwaka 2009 Sofapaka FC walisajili ushindi wa magoli 3 – 1 dhidi ya mwenyeji na bingwa mwaka 1963 Nakuru AllStars aliyepata bao la kipekee kupitia Boniface Akenga huku Collins Shivachi, aliyetimiza miaka 23 leo, na mawili kutoka kwa kigogo John Baraza yakimshindia Sam Timbe mechi yake ya pili msimu huu.
    Nazo mechi sita ziligaragazwa siku ya Jumamosi ambapo SoNy Sugar waliwapiku Bandari 1 – 0 (Mombasa), Muhoroni Youth 2 – 2 Tusker FC (Muhoroni), Mathare United 0 – KCB FC, Ushuru FC 0 – 0 Ulinzi Stars, zote Nyayo, huku Chemelil Sugar ikitoa sare ya 1 – 1 na City Stars nao Thika United wakamshangaza Western Stima kwa ushindi wa 1 – 0, mechi hizi mbili zikiandaliwa uwanjani Kisumu.
    Kwenye ligi ya Shirikisho la Soka Kenya, FKF, inayopeperushwa na Azam TV, mechi tisa zilipepetwa wikiendi hii na haya ndiyo matokeo.

    MATOKEO KAMILI MECHI ZA LIGI YA AZAM TV KENYA;

    JUMAPILI
    Finlays Horticulture 1 – 1 Nakumatt FC
    Agrochemicals 3 – 1 FC Talanta
    Zoo Kericho 2 – 1 West Sugar
    MOSCA FC 0 – 4 Kakamega Homeboyz
    Modern Coast Rangers 1 – 1 Bidco United

    JUMAMOSI
    Ligi Ndogo 0 – 2 Posta Rangers
    St. Josepg 2 – 1 Nairobi Stima
    Kariobangi Sharks 1 – 2 Nzoia United
    Oserian FC 0 – 1 Shabana FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'DEBI' LA MASHEMEJI KENYA LAISHIA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top