• HABARI MPYA

  Monday, May 01, 2023

  YANGA SC WAENDA SINGIDA KWA MECHI MBILI KATI YA TATU NDANI YA SIKU SABA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameondoka Dar es Salaam leo kwa ndege kwenda Singida kwa ajili ya mechi mbili mfululizo dhidi ya wenyeji, Singida Big Stars Alhamisi na Jumapili.
  Yanga inakabiliwa na ratiba ngumu mno ya kucheza mechi tatu za mashindano tofauti ndani ya siku saba katika miji miwili, Singida na Dar es Salaam.
  Alhamisi itakuwa mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Jumapili Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zote dhidi ya Singida Uwanja wa LITI.
  Baada ya hapo watasafiri kurejea Dar es Salaam kwa mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini Jumatano ijayo, Mei 10.
  Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu, Yanga imebakiza jumla mechi nne za Ligi Kuu pamoja na huo wa Singida Big Stars, nyingine dhidi ya Dodoma Jiji, Mbeya City na Tanzania Prisons zote ugenini na wanatakiwa kushinda mechi tatu ili kuwa mabingwa tena.
  Mechi ya marudiano na Marumo Gallants itafanyika Afrika Kusini Mei 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAENDA SINGIDA KWA MECHI MBILI KATI YA TATU NDANI YA SIKU SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top