• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 05, 2020

  SIMBA SC YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA, SASA KUMENYANA NA PLATINUM FC YA ZIMBABWE

  Na Mwandishi Wetu, DARES SALAAM
  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kuingia Hatua ya 32 Bora michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na Plateau United ya Nigeria katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa 1-0 ulioupata kutokana na bao pekee la Mzambia, Clatous Chama kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa Kimataifa wa Jos, Nigeria.
  Sasa Wekundu wa Msimbazi watamenyana na Platinum FC ya Zimbabwe iliyoitoa Costa do Sol ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 4-1 ikishinda 2-1 ugenini wiki iliyopita na 2-0 leo Bulawayo.  


   
  Mechi ya kwanza itachezwa Jumanne ya Desemba 22 mjini Bulawayo na marudiano yatafuatia Jumatano ya Januari 6 Dar es Salaam.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga/Bernard Morrison dk69, Muzamil Yassin, John Bocco/Meddie Kagere dk90, Clatous Chama na Luis Miquissone.
  Plateau United; Adamu Abubakar, Abubakar Ibrahim, Gabriel Wassa, Dennis Nya, Andrew Ikefe/Elisha Golbe dk77, Isah Ndala/Innocent Kingsley dk88, Oche Ochewechi, Sunday Adetunji, Abba Umar, Ibrahim Buhari, Henlong Henry.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA, SASA KUMENYANA NA PLATINUM FC YA ZIMBABWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top