• HABARI MPYA

  Friday, December 18, 2020

  AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA RUVU CHAMAZI, BIASHARA YAITANDIKA MBEYA CITY 3-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Sare hiyo inaifanya Azam FC ifikishe pointi 29 baada ya kucheza mechi 16, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 32 za mechi 14 na vinara, Yanga SC wenye pointi 37 za mechi 15. 
  Mara mbili Azam FC walitangulia kwa mabao ya Ayoub Lyanga dakika ya 34 na Mudathir Yahya dakika ya 60 na Ruvu Shooting ilisawazisha kupitia kwa Emmanuel Martin dakika ya 53 na Fully Zulu Maganga dakika ya 70.  

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Biashara United imeichapa Mbeya City 3-0, mabao ya Chrustian Zigah dakika ya 10 na 25 na Derick Mussa dakika ya 68 Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Kagera Sugar wakaibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Nassor Kapama dakika ya 56, Peter Mwalyanzi dakika ya 73 na Saadat Mohamed dakika ya 80, wakati la Coastal Union limefungwa na Abdul Suleiman dakika ya 45 kwa penalti.   
  Mchezo uliotangulia mchana bao la dakika ya 90 la Salum Chubi liliinusuru Mwadui FC kulala nyumbani mbele ya Polisi Tanzania iliyotangulia kwa bao la Daruwesh Saliboko dakika ya 17 Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA RUVU CHAMAZI, BIASHARA YAITANDIKA MBEYA CITY 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top