• HABARI MPYA

  Friday, December 11, 2020

  ARSENAL WAMALIZA NA USHINDI WA 4-2 UGENINI EUROPA LEAGUE


  TIMU ya Arsenal imekamilisha hatua ya makundi ya UEFA Europa League  kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Dundalk FC usiku wa jana Uwanja wa Aviva Jijini Dublin.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Eddie Nketiah dakika ya 12, Mohamed Elneny dakika ya 18, Joe Willock dakika ya 67 na Folarin Balogun dakika ya 80, wakati ya Dundalk FC yamefungwa na Jordan Flores dakika ya 22 na Sean Hoare dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo, Arsenal imemaliza na pointi 18, ikifuatiwa na Molde yenye pointi 10, Rapid Wien pointi saba, wakati Dundalk haina pointi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL WAMALIZA NA USHINDI WA 4-2 UGENINI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top