• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2020

  NADO APIGA MBILI AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA 2-2 NA NAMUNGO FC CHAMAZI

  TIMU ya Azam FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Namungo FC ya Ruangwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
  Mara mbili winga Iddi Suleiman ‘Nado’ aliitanguza Azam FC dakika ya 19 na 74, lakini mar azote Namungo FC ikasawazisha kupitia kwa beki Edward Charles Manyama dakika ya 25 na mshambuliaji Mghana, Stephen Sey dakika ya 90 na ushei.
  Na kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 15 na inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 29 za mechi 13 na Yanga SC wenye pointi 37 za mechi 15 pia.


  Namungo FC wamefikisha pointi 17 baada ya kucheza mechi 13 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 13 kwenye ligi ya 18, ambayo mwisho wa msimu timu nne zitashuka na mbili zitamenyana na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubaki Ligi Kuu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NADO APIGA MBILI AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA 2-2 NA NAMUNGO FC CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top