• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 10, 2020

  NYOTA WA KIKOSI CHA ITALIA 1982 PAOLO ROSSI AFARIKI DUNIA

  NYOTA wa kikosi cha Italia kilichotwaa Kombe la Dunia 1982 nchini Hispania, Paolo Rossi amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 64.
  Kifo cha mshambuliaji huyo wa zamani wa Juventus na AC Milan,  aliyetwaa Mpira wa Dhahabu na Kiatu cha Dhahabu mwaka 1982 ambaye aliichezea mechi 48 nchi yake, kimetangazwa mapema leo na Televisheni ya RAI Sport ya kwao, Italia ambayo Rossi alikuwa anaifanyia kazi kama Mchambuzi.
  Rossi ameshinda mataji mawili ya Serie A, moja la Ulaya na Coppa Italia katika miaka yake minne Juve – lakini zaidi mchango wake kwa timu ya taifa  ndio unakumbukwa mno, mabao yake sita yakiipa Italia Kombe nchini Hispania miaka 38 iliyopita.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NYOTA WA KIKOSI CHA ITALIA 1982 PAOLO ROSSI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top