• HABARI MPYA

  Friday, December 11, 2020

  YANGA SC TAYARI WAPO SHINYANGA KWA AJILI YA MCHEZO NA MWADUI FC KESHO KAMBARAGE


  KIKOSI cha Yanga SC tayari kipo Shinyanga kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC kesho Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

  Wamesafiri kwa ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambao wamepanda basi hadi Shinyanga. 

  Yanga SC tayari imevuna pointi 10 katika mechi zake nne za awali za kanda ya Ziwa, ikizifunga 1-0 zote Kagera Sugar mjini Bukoba na Biashara United mjini Musoma na KMC 2-1 mjini Mwanza kabla ya sare ya 1-1 na Gwambina FC wilayani Misungwi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC TAYARI WAPO SHINYANGA KWA AJILI YA MCHEZO NA MWADUI FC KESHO KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top