• HABARI MPYA

  Wednesday, December 30, 2020

  KAGERE APIGA MBILI, TSHABALALA NA MUGALU MOJA KILA MMOJA SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 4-0 DAR

  MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbila ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa Ihefu SC 4-0 jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck inafikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 15, ingawa inabaki nafasi ya pili mbele ya vinara, Yanga SC wenye pointi 43 za mechi 17.
  Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Nassor Mwinchui wa Pwani aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Geoffrey Msakila wa Geita hadi mapumziko SImba SC walikuwa mbele kwa mabao 3-0.


  Leo biashara ilifunguliwa na beki wa kulia, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dakika ya tisa akimalizia kazi nzuri ya beki wa kulia, Shomari Kapombe, wote wazawa.
  Mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu misimu miwili mfululizo iliyopita akaifungia Simba SC mabao mawili dakika ya 15 akimalizia pasi ya winga Luis Miqussion kutoka Msumbiji na dakika ya 40 akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama.
  Mshambuliaji mpya, Chris Mutshimba Kope Mugalu, raia wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo (DRC) akakamilisha shagwe za mabao dakika ya 84 akimalizia pasi ya Chama.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Ibrahim Ame/David Kameta dk72, Kennedy Juma, Rally Bwalaya, Said Ndemla, Meddie Kagere/Chriss Mugalu dk66, Clatous Chama na Luis Miquissone/Hassan Dilunga dk75.
  Ihefu SC; Deo Munishi ‘Dida’, Mando Mkubwa, Omary Kindamba, Wema Sadoki, Michael Masinda, Samuel Jackson, Juma Mahadhi/Issa Ngoah dk47, Willy Mgaya, Andrew Simchimba/ Teps Evance dk90, Omary Hamisi/Joseph Kinyozi dk47 na Joseph Mahundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERE APIGA MBILI, TSHABALALA NA MUGALU MOJA KILA MMOJA SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 4-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top