• HABARI MPYA

  Friday, December 18, 2020

  MTOTO WA KWANZA WA WAYNE ROONEY ASAINI MANCHESTER UNITED


  MTOTO mkubwa wa Nahodha wa zamaani wa Manchester united, Wayne Rooney, Kai amesaini mkataba wa kujiunga na timu ya vijana ya klabu hiyo.
  Rooney ameposti picha akiwa na mkewe, Coleen wakimshuhudia mtoto wao wa umri wa miaka 11, Kai akisaini.

  Katika miaka yake 13 ya kuwa na Mashetani hao Wekundu, Rooney ameweka rekodi ya Ufungaji Bora wa muda wote wa klabu kwa mabao yake 253, akiiwezesha timu kushinda mataji matano ya Ligi Kuu, moja la Champions League na mengineyo
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTOTO WA KWANZA WA WAYNE ROONEY ASAINI MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top