• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 16, 2020

  BENZEMA APIGA MBILI REAL MADRID YAICHAPA BILBAO 3-1


  Mshambuliaji Karim Benzema jana amefunga mabao mawili Real Madrid ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye mchezo wa La Liga Uwanja wa Alfredo Di Stéfano.
  Benzema alifunga mabao mawili dakika za 74 ba 90 na ushei, baada ya Toni Kroos kufunga la kwanza dakika ya 45 , huku bao la wageni likifungwa na Capa dakiaka ya 52.
  Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi 26 sawa na vinara, Real Sociedad baada ya wote kucheza mechi 13. Atletico Madrid pia ina ponti 26, ingawa yenyewe imecheza mechi 11 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BENZEMA APIGA MBILI REAL MADRID YAICHAPA BILBAO 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top