BAO pekee la kiungo Salum Kihimbwa limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 15 na kupanda nafasi ya tisa kutoka ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakati KMC inayobaki na pointi zake 21za mechi 13 sasa inabaki nafasi ya tano.
0 comments:
Post a Comment