• HABARI MPYA

  Friday, December 25, 2020

  SIMBA SC WAPANGWA NA MTIBWA, CHIPUKIZI KUNDI B, YANGA NA NAMUNGO NA JAMHURI KOMBE LA MAPINDUZI 2021

  MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC ya Dar es Salaam wamepangwa Kundi B katika Kombe la Mapinduzi pamoja na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar ya Morogoro na Chipukizi FC ya Pemba.
  Vigogo Yanga SC ya Dar es Salaam pia wamepangwa Kundi A pamoja na Namungo FC ya Lindi na Jamhuri FC ya Pemba pia.
  Kundi C linazikutanisha Azam FC ya Dar es Salaam na vigogo wa visiwani, Malindi FC na  Mlandege FC  ambao ndio mabingwa wa Zanzibar. 
  Michuano hiyo itaanza Januari 5, mwakani Yanga SC ikimenyana na Jamhuri usiku baada ya Mtibwa Sugar kucheza na Chipukizi jioni.


  RATIBA KAMILI KOMBE LA MAPINDUZI
  Januari 5, 2021
  Yanga SC v Jamhuri
  Mtibwa Sugar v Chipukizi
  Januari 6, 2021
  Malindi FC v Mlandege
  Januari 7, 2021
  Simba SC v Chipukizi
  Januari 8, 2021
  Azam FC v Mlandege FC
  Yanga SC v Namungo FC
  Januari 9, 2021
  Jamhuri FC v Namungo FC
  Simba SC v Mtibwa sugar
  Januari 10, 2021
  Azam FC v Malindi FC
  ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
  Mwaka    Bingwa Mshindi wa Pili
  2007 Yanga SC Mtibwa Sugar 
  2008 Simba SC Mtibwa Sugar
  2009 Miembeni        KMKM
  2010 Mtibwa Sugar         Ocean View
  2011 Simba SC  Yanga SC
  2012 Azam FC          Simba SC
  2013 Azam FC    Tusker FC
  2014 KCCA        Simba SC
  2015 Simba SC Mtibwa Sugar
  2016 URA Mtibwa Sugar
  2017 Azam FC Simba SC
  2018 Azam FC URA FC
  2019 Azam FC Simba SC 2-1 
  2020 Mtibwa Sugar         Simba SC 1-0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPANGWA NA MTIBWA, CHIPUKIZI KUNDI B, YANGA NA NAMUNGO NA JAMHURI KOMBE LA MAPINDUZI 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top