• HABARI MPYA

  Thursday, December 24, 2020

  ULIMWENGU APIGA MBILI TP MAZEMBE YAICHAPA BOUENGUIDI FC 2-1 KWAO LIGI YA MABINGWA

  MSHAMBUILIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu jana amefunga mabao mawili kuiwezesha TP Mazembe kupata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Bouenguidi FC Uwanja wa Augustin Monédan de Sibang mjini Libreville, Liberia.
  Ulimwengu alifunga mabao hayo dakika ya 28 na 63, wakati bao la Bouenguidi FC lilifungwa na Junhior Bayanho Aubiang dakika ya 17.
  Mtanzania mwingine, Simon Msuva, klabu yake Wydad Athletic ilichapwa 1-0 na Stade Malien jana Uwanja wa Stade 26 Mars Jijini Bamako, Mali katika mchezo mwingine wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ULIMWENGU APIGA MBILI TP MAZEMBE YAICHAPA BOUENGUIDI FC 2-1 KWAO LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top