• HABARI MPYA

  Sunday, December 20, 2020

  ARSENAL YAENDELEA KUBORONGA ENGLAND, YAPIGWA 2-1 NA EVERTON


  NAYE kocha Mikel Arteta amezidi kujikuta katika wakati mgumu Arsenal baada ya timunhiyo kuendelea kuboronga kufuatia kuchapwa mabao 2-1 na Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Goodison Park.
  Mabao ya Everton yalifungwa na Rob Holding aliyejifunga dakika ya 22 na Yerry Mina dakika ya 46, wakati la Arsenal Nicolas Pepe kwa penalti dakika ya 35.
  Everton inafikisha pointi 26 na kupanda nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Liverpool baada ya wote kucheza mechi 14, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 14 za mechi 14 nafasi ya 15
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAENDELEA KUBORONGA ENGLAND, YAPIGWA 2-1 NA EVERTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top