• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2020

  MAN UNITED NA REAL SOCIEDAD, ARSENAL NA BENFICA EUROPA LEAGUE


  Manchester United itamenyana na vinara wa LaLiga, Real Sociedad katika hatua ya 32 UEFA Europa League
   

  RATIBA KAMILI

  Wolfsberger AC vs Tottenham Hotspur

  Dynamo Kyiv vs Club Brugge

  Real Sociedad vs Manchester United

  Benfica vs Arsenal

  Crvena Zvezda vs AC Milan

  Royal Antwerp vs Rangers

  Slavia Prague vs Leicester City

  Salzburg vs Villarreal

  Braga vs Roma

  Krasnodar vs Dinamo Zagreb

  Young Boys vs Bayer Leverkusen

  Molde vs Hoffenheim

  Granada vs Napoli

  Maccabi Tel-Aviv vs Shakhtar Donetsk

  Lille vs Ajax

  Olympiacos vs PSV Eindhoven

  Mechi za kwanza zitachezwa Alhamisi ya Februari 18; marudiano Alhamisi ya Februari 25

  TIMU ya Manchester United itamenyana na vinara wa LaLiga, Real Sociedad katika hatua ya 32 UEFA Europa League.
  Baada ya kuangukia kwenye michuano hiyo kufuatia kutolewa katika Ligi ya Mabingwa, kocha Ole Gunnar Solskjaer atakabiliwa na matihani mwingine mgumu mbele ya timu inayoongoza kwa kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya Hispania kwa sasa.
  Arsenal nay imeoangiwa mpinzani mgumu katika Hatua hii, ambayo ni Benfica ya Ureno huo ukiwa mtihani mwingine kwa kocha Mikel Arteta kufuatia matokeo mabaya mfululizo msimu huu.
  Kocha maarufu, Mreno Jose Mourinho kidogo hatakuwa na kazi ngumu baada ya Tottenham Hotspur kupangiwa Wolfsberger ya Austria.
  Mechi ya Tottenha itachezwa Saa 24 kabla ya nyingine Jumatano ya Februari 24, kwa sababu Arsena watakuwa wana mechi pia, hivyo Jiji la London haliwezi kuwa na michezo miwili ya Europa League wakati mmoja.
  Leicester City ni timu nyingine iliyopata mpinzani mwepesi kidogo, kwani itamenyana na Slavia Prague.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED NA REAL SOCIEDAD, ARSENAL NA BENFICA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top