• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2020

  NGORONGORO HEROES WAPIGWA 1-0 NA WENYEJI SAUDIA ARABIA KATIKA MECHI YA KIRAFIKI LEO

  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo imefungwa 1-0 na wenyeji, Saudi Arabia katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Chuo Kikuu cha Prince Muhammad Bin Fahd mjini Khobar.
  Ushindi huo unamaanisha Saudi Arabia imelipa kisasi cha kuchapwa 1-0 na kikosi cha kocha Jamhuri Kihwelo katika mchezo wa kwanza Alhamisi.
  Ngorongoro Heroes imetumia ziara ya Saudi Arabia kama ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) chini ya umri wa miaka 20 zitakazofanyika Mauritania kuanzia Februari 14 hadi Machi 4, mwakani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES WAPIGWA 1-0 NA WENYEJI SAUDIA ARABIA KATIKA MECHI YA KIRAFIKI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top