• HABARI MPYA

  Sunday, December 20, 2020

  SERENGETI BOYS YAFUZU AFCON U17 BAADA YA KUITOA ETHIOPIA KWA MATUTA NUSU FAINALI CECAFA U17

  TANZANIA imefanikiwa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Ethiopia kufuatia sare ya 1-1 leo kwenye mchezo wa Nusu Fainali Uwanja wa Umuganda mjini Rubavu, Rwanda.
  Sasa Tanzania itamenyana na mabingwa watetezi, Uganda katika fainali Jumanne hapo hapo Uwanja wa Umuganda. The Cubs wao wameingia fainali baada ya kuitoa Djibouti mapema leo mchana hapo hapo Umuganda
  Serengeti Boys sasa itashiriki Fainali za AFCON U17 kwa mara ya tatu mfululizo Julai mwakani nchini Morocco baada ya 2017 Gabon na 2019 walipokuwa wenyeji.


  Na Serengeti Boys, mabingwa wa CECAFA U-17 mwaka 2108 nchini Burundi, wanafuata nyayo za kaka zao, Ngorongoro Heroes waliofuzu Fainali za AFCON U-20 zitakazofanyika nchini Mauritania kuanzia Februari 14 hadi Machi 4 mwakani.
  Tanzania walikuwa wenyeji wa CECAFA U-20 mwishoni mwa Novemba na wakamaliza nafasi ya pili baada ya kufungwa 4-1 na Uganda Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu mkoani Arusha Desemba 2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAFUZU AFCON U17 BAADA YA KUITOA ETHIOPIA KWA MATUTA NUSU FAINALI CECAFA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top