• HABARI MPYA

  Tuesday, December 22, 2020

  BIASHARA UNITED YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-0 MUSOMA NA KUPANDA NNE BORA LIGI KUU

  TIMU ya Biashara United leo imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo Deo Mafie dakika ya 55 na Kelvin Friday dakika ya 90 na kwa ushindi huo, Biashara United inayofundishwa na beki wa zamani wa Yanga, Mkenya Francis Baraza inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 17 na kupanda hadi nafasi ya nne ikizidiwa pointi tatu na Azam FC iliyocheza mechi 16.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao la dakika ya 90 la kiungo wa zamani wa Simba, Peter Mwalyanzi limeinusuru Kagera Sugar kupoteza mechi nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Polisi Tanzania Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. 


  Kagera Sugar ilitangulia kwa bao la Ally dakika ya 11, lakini Polisi Tanzania ikasawazisha kupitia kwa Daruwesh Saliboko dakika ya 24 na kupata la pili dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Tariq Seif Kiakala.
  Nayo Mwadui FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga.
  Mapema mchana wa leo, bao la dakika ya mwisho kabisa la Japhet Mayunga liliinusuru Gwambina kuchapwa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City, waliotangulia kwa bao la penalti la Kibu Dennis dakika ya 34.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-0 MUSOMA NA KUPANDA NNE BORA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top