• HABARI MPYA

  Friday, December 25, 2020

  MSHAMBULIAJI MZIMBABWE WA AZAM FC, PRINCE DUBE AANZA KUJIFUA CHINI YA KOCHA WA MAZOEZI YA VIUNGO

  MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube Mpumelelo ameanza programu maalumu ya mazoezi ya kujiweka sawa, chini ya Kocha wa viungo wa klabu hiyo, Nyasha Charandura.
  Dube aliyejiunga na Azam FC mwanzoni mwa msimu, yupo nje maumivu ya mkono wake wa kushoto alioumia Novemba 25 wakifungwa 1-0 na Yanga na anatarajiwa kurejea dimbani Januari 15, mwakani.
  Kabla ya kurejea kwenye ushindani, Dube atafanyiwa kipimo cha X-Ray kuangalia maendeleo ya mkono wake.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI MZIMBABWE WA AZAM FC, PRINCE DUBE AANZA KUJIFUA CHINI YA KOCHA WA MAZOEZI YA VIUNGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top