• HABARI MPYA

  Wednesday, December 23, 2020

  SIMBA SC YATELEZA ZIMBABWE, YACHAPWA 1-0 NA FC PLATINUMS HARARE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  BAO pekee la Perfect Chikwende dakika ya 17 limaipa ushindi wa 1-0 FC Platinums dhidi ya Simba SC ya Tanzania katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Harare nchini Zimbabwe.
  Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Chris Mutshimba Mugalu aliukwamisha nyavuni mpira dakika ya 78 akimalizia kazi nzuri ya kiungo mzawa, Hassan Dilunga, lakini mwamuzi akakataa bao hilo akisema mfungaji alikuwa ameotea.
  Simba SC sasa itahitaji ushindi wa tofauti ya mabao mawili nyumbani Januari 6 ili kwenda Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo inayochezwa kwa mtindo wa makundi.
  Timu itakayotolewa itamenyana na moja ua timu zitakazovuka Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho kuwania kucheza Hatua ya makundi ya michuano hiyo midogoya ngazi ya klabu barani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATELEZA ZIMBABWE, YACHAPWA 1-0 NA FC PLATINUMS HARARE LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top