• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 06, 2020

  MAN UNITED YATOKEA NYUMA NA KUICHAPA WEST HAM 3-1 LONDON


  TIMU ya Manchester United jana imetokea nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya wenyeji, West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa London. 
  West Ham walitangulia kwa bao la Tomas Soucek dakika ya 38, kabla ya Man United kuzinduka kwa mabao ya Paul Pogba dakika ya 65, Mason Greenwood dakika ya 68 na Marcus Rashford dakika ya 78.
  Kwa ushindi huo, Mashetani Wekundu wanafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 10 na kupanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya nne, wakizidiwa pointi tatu na vinara, Chelsea ambao hata hivyo wana mchezo mmoja zaidi, wakati West Ham inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya saba baada ya mechi 11
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOKEA NYUMA NA KUICHAPA WEST HAM 3-1 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top