• HABARI MPYA

  Sunday, December 20, 2020

  AZAM FC YAUZA MCHEZAJI WA TATU NDANI YA NUSU MSIMU, AKONO ANUNULIWA NA KLABU YA MALAYSIA

  MSHAMBULIAJI Mcameroon wa Azam FC,  Alain Thierry Akono Akono amejiunga na klabu ya Negeri Sembilan ya Malaysia.
  Taarifa ya Azam FC kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba, wamefanikiwa kumuuza mchezaji huyo baada ya nusu msimu wa kuwa naye. 
  Akono alijiunga na Azam FC mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya AS Fortuna ya Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili. 


  Akono anakuwa mchezaji wa tatu kuuzwa na Azam FC msimu huu baada ya kiungo Novatus Dissmas aliyejiunga na Maccabi Tel-Aviv ya Israel na mshambuliaji Shaaban Idd Chilunda aliyejiunga na Moghreb Atletic Tetouan Morocco ya Morocco.
  Pamoja na hayo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Azam FC, Thabit Zakaria 'Zaka Zakazi' amesema klabu itafanya usajili kabla ya dirisha dogo kufungwa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAUZA MCHEZAJI WA TATU NDANI YA NUSU MSIMU, AKONO ANUNULIWA NA KLABU YA MALAYSIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top