• HABARI MPYA

    Wednesday, December 23, 2020

    NAMUNGO FC WANG'ARA AFRIKA, WAICHAPA AL HILAL OBAYED YA SUDAN 2-0 CHAMAZI KOMBE LA SHIRIKISHO

    MABAO ya Sixtus Sabilo dakika ya 14 na Stephen Sey dakika ya 31 yameipa Namungo FC ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Hilal Obayed ya Sudan jioni ya leo katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika.
    Sasa Namungo FC itatakiwa kwenda kulazimisha sare ugenini au kufungwa si kwa zaidi ya tofauti ya bao moja ili kusonga mbele, ambako watamenyana na moja ya timu zitakazotolewa Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
    Kama ilivyo katika Ligi ya Mabingwa, Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho huhusisha pia timu 16 zinazogawanywa kwenye makundi manne.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAMUNGO FC WANG'ARA AFRIKA, WAICHAPA AL HILAL OBAYED YA SUDAN 2-0 CHAMAZI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top