• HABARI MPYA

  Sunday, December 27, 2020

  MABONDIA WA TANZANIA WAADHIBU WAGENI KWA VIPIGO TOFAUTI DAR

  MABONDIA nyota wa Tanzania jana waliwashinda wapinzani wao kutoka nchi tofauti kwa staili mbalimbali katika ukumbi wa Next Door Arena – Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ akiwa kivutio zaidi baada ya kumshinda Symon Tcheta wa Malawi kwa KO raundi ya kwanza.
  Mfaume Mfaume alishinda kwa pointi dhidi ya Chikondi Makawa wa Malawi sawa Ismail Galiatano aliyemshinda Israel Kamwamba wa Malawi pia, wakati Tonny Rashid alimpiga Hassan Milanzi wa Zimbabwe kwa KO raundi ya pili, Selemani Kidunda akamchapa Limbani Masamba wa Malawi pia kwa KO raundi ya pili.
  Mpinzani wa Twaha Kiduku, Guy Tshimanga Tshitundu kutoka Kongo hakutokea, wakati Juma Choki akamchaka Issa Nampepeche kwa TKO raundi ya tatu katika pambano la watoto wa nyumbani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABONDIA WA TANZANIA WAADHIBU WAGENI KWA VIPIGO TOFAUTI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top