• HABARI MPYA

  Tuesday, December 15, 2020

  NTIBANZOKIZA AANZA NA MABAO MAWILI YANGA SC YAWACHAPA SINGIDA UNITED 3-0 MECHI YA KIRAFIKI

  YANGA SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Singida United jioni ya leo Uwanja wa Malkia Liti, Singida.  
  Mchezaji mpya, Saido Ntibanzokiza amefunga mabao mawili dakika ya 22 akimalizia pasi ya farid Mussa Malik na la p[ili dakika ua 66 kwa penalti baada ya Ditram Nchimbi kuangushwa.
  Nyota ya kiungo mzawa, Deus Kaseke imeendelea kung'ara leo kufuatia kuifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 82 mara tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Ntibanzokiza akimalizia pasi ya Farid Mussa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NTIBANZOKIZA AANZA NA MABAO MAWILI YANGA SC YAWACHAPA SINGIDA UNITED 3-0 MECHI YA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top