• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 20, 2020

  SIMON MSUVA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO WYDAD CASABLANCA YAICHAPA 3-0 HASSANIA AGADIR

  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefunga bao lake la kwanza katika klabu yake mpya, Wydad Athletic ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Hassania Agadir katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro Uwanja wa Mohamed V,  Casablanca.
  Msuva alifunga bao la pili dakika ya 53, baada ya Muaid Salem Ali kufunga la kwanza dakika ya 43 na  Ayoub El Amloud akafunga la tatu dakika ya 90 na kwa ushindi huo, Wydad inafikisha pointi tisa na kupanda nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja na Raja baada ya wote kucheza mechi nne.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMON MSUVA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO WYDAD CASABLANCA YAICHAPA 3-0 HASSANIA AGADIR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top