• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 22, 2020

  TANZANIA YAENDELEA KUTESEKA KWA WAGANDA, SERENGETI BOYS YATANDIKWA 3-1 NA CUBS RWANDA

  TANZANIA imeendeleza unyonge kwa Uganda kwenye soka baada ya Serengeti Boys leo kuchapwa mabao 3-1 na Cubs katika fainali ya CECAFA U-17 Uwanja wa Umuganda mjini Rubavu, Rwanda.
  Kipigo hicho kinawakumbusha Watanzania machungu ya kukosa Kombe la CECAFA U-20 wakiwa wenyeji baada ya kufungwa 4-1 na Uganda Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu mkoani Arusha Desemba 2.
  Lakini kama ilivyokuwa kwenye CECAFA U-20, timu zinazokutana kwenye fainali ya michuano hiyo ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati moja kwa moja zinakuwa zimefuzu fainali za Afrika – maana yake Uganda na Tanzania zitashiriki AFCON U-17 na U-20 mwakani.


  Fainali za AFCON U17 zitafanyika Julai mwakani nchini Morocco, wakati za AFCON U-20 zitafanyika Mauritania kuanzia Februari 14 hadi Machi 4 mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA YAENDELEA KUTESEKA KWA WAGANDA, SERENGETI BOYS YATANDIKWA 3-1 NA CUBS RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top