• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 05, 2020

  KAGERA SUGAR YAWACHAPA TANZANIA PRISONS 1-0, SUMBAWANGA COASTAL UNION 0-0 MBEYA CITY TANGA

  Na Mwandishi Wetu, SUMBAWANGA
  BAO pekee la Hassan Mwaterema dakika ya 63 leo limewapa ushindi wa 1-0 Kagera Sugar dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inayofundishwa na Mecky Mexime Silili Kianga, Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 14 na kupanda hadi nafasi ya tisa kutoka ya 13, wakati Tanzania Prisons inabaki nafasi ya saba na ponti zake 19 za mechi 14 pia.  
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. 


  Coastal inafikisha pointi 17 baada ya mechi 14 na inasogea nafasi ya tisa kutoka ya 11, wakati Mbeya City inafikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi ingawa inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 18, ambayo mwisho wa msimu nne zitashuka na mbili zitakwenda kucheza na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubaki. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAWACHAPA TANZANIA PRISONS 1-0, SUMBAWANGA COASTAL UNION 0-0 MBEYA CITY TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top