• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2020

  BARCA NA PSG, RONALDO ARUDISHWA URENO 16 BORA LIGI YA MABINGWA

  MABINGWA watetezi, Bayern Munich watamenyana na Lazio ya Italia katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.
  Chelsea itamenyana na Atletico Madrid, wakati Liverpool wataivaa RB Leipzig na Manchester City itacheza na Borussia Monchengladbach.
  Barcelona ya Lionel Messi itamenyana na Paris Saint-Germain ya Neyamr, wakati Cristiano Ronaldo ataiongoza Juventus dhidi ya Porto ya nyumbani kwao, Ureno.
  Lionel Messi (kulia) ataiongoza Barcelona dhidi ya PSG iliyofika fainali na kufungwa na Bayer Munich msimu uliopita 

  Mechi nyingine za hatua hiyo Sevilla itamenyana na Borussia Dortmund, wakati mabingwa mara 13, Real Madrid watamenyana na Atalanta.

  Mechi za kwanza zitachezwa na kati ya Februari 16, 17 na 23 na 24 , na za marudiano zitachezwa kati yaMachi 9 na 10 na 16 na 17 mwakani, 2021.
  RATIBA KAMILI
  Gladbach v Man City
  Lazio v Bayern
  Atletico v Chelsea
  Leipzig v Liverpool
  Porto v Juventus
  Barcelona v PSG
  Sevilla v Dortmund
  Atalanta v Real Madrid
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCA NA PSG, RONALDO ARUDISHWA URENO 16 BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top