• HABARI MPYA

  Sunday, December 27, 2020

  SIMBA SC YAIFUMUA MAJI MAJI YA SONGEA 5-0 NA KUSONGA MBELE AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  MABINGWA watetezi, Simba SC wamesonga mbele michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Maji Maji ya Songea usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Mabao ya Simba SC katika mchezo wa leo yamefungwa na beki mzawa Gardiel Michael dakika ya tatu, mshambuliaji Mkongo Chris Mugalu dakika ya sita, beki Mzanzibari Ibrahim Ame dakika ya 60, mshambuliaji Mrwanda Meddie Kagere dakika ya 78 na kiungo kutoka Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 90.
  Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar iliilaza 1-0 Geita Gold, bao pekee la Ismail Mhesa dakika ya 67 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Beno Kakolanya, David Kameta, Gardiel Michael, Ibrahim Ame, Kennedy juma, Said Ndemla/Shomari Kapombe dk66, Miraj Athumani ‘Madenge’, Rally Bwalya/Luis Miquissone dk66, Ibrahim Ajibu, Chris Mugalu/Meddie Kagere dk65 na Francis Kahata.
  Maji Maji; Mputi Jaffar, Juma Abdallah, Felix Stephen/Abdallah Mapunda dk33, Jackson Brighton, Idrisa Mohammed, Mfaume Mfaume, Nicolas Mapunda, Kashiru Salum, Arafat Arafat, Ismail Mussa na Hamidu Omary.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIFUMUA MAJI MAJI YA SONGEA 5-0 NA KUSONGA MBELE AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top