• HABARI MPYA

  Monday, December 28, 2020

  BEKI MKONGWE NCHINI KELVIN YONDAN ALIYEACHWA NA VIGOGO, YANGA SC ASAJILIWA NA POLISI TANZANIA

  Na Clement Shari, ARUSHA
  KLABU ya soka ya Polisi Tanzania yenye maskani yake mjini Moshi mkoani Kilimanjaro imetangaza kumsajili beki wa zamani wa klabu ya Yanga Kelvin Patrick Yondan katika dirisha hili dogo ambalo kwa sasa lipo wazi.
  Msemaji wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro kwa njia ya ujumbe wa Sauti alioutuma kwa wanahabari amesema mchezaji huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Polisi Tz.
  Lukwaro amesema tayari mchezaji huyo amekwishakutua mjini Moshi kuanza majukumu kwenye timu yake mpya Mara baada ya kukaa nje ya dimba kwa nusu msimu.


  Wiki iliyopita zilikuwepo tetesi za mchezaji huyo kusajiliwa na Polisi lakini uongozi wa timu hiyo haukuwa tayari kuweka mambo hadharani.
  Lukwaro amesema klabu ya Polisi italitumia dirisha hili dogo kukiimarisha kikosi chake bila ya kutaja ni wachezaji gani wanaotaraji kuwasajili na nafasi zao za uwanjani.
   Mpaka sasa klabu ya Polisi Tz ipo katika nafasi ya 6 ikiwa na alama 23 Mara baada ya kucheza michezo 17 ya Mzunguko wa kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI MKONGWE NCHINI KELVIN YONDAN ALIYEACHWA NA VIGOGO, YANGA SC ASAJILIWA NA POLISI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top