• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 28, 2020

  SIMBA SC YAMSIMAMISHA JONAS MKUDE KWA MUDA USOJULIKANA KUTOKANA NA UTOVU WA NIDHAMU


  KLABU ya Simba SC imemsimamisha kwa muda usiojulikana kiungo wake Jonas Mkude kutokana na utovu wa nidhamu.
  Taarifa iliyotolewa na mtendaji mkuu wa klabu hiyo kwa vyombo vya habari imesema Mkude amesimamishwa ili kupisha kusikilizwa kwa tuhuma zinazomkabili mchezaji huyo bila kutaja ni tuhuma zipi huku swala lake likipelekwa katika kamati ya nidhamu ya timu hiyo.
  Taarifa hiyo imesema klabu hiyo haitaweza kuvumilia kwa namna yoyote vitendo vya utovu wa nidhamu na kudai nidhamu ndo uti wa mgongo wa mafanikio ya klabu hiyo.
  Vitendo alivyovifanya Jonas Mkude itakuwa ni pigo kwa klabu hiyo ya Msimbazi inayokabiliwa na mchezo muhimu wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Platinum ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa mwanzoni mwa mwezi ujao jijini Dar Es Salaam.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMSIMAMISHA JONAS MKUDE KWA MUDA USOJULIKANA KUTOKANA NA UTOVU WA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top